Sheria ya TIN Mitandaoni Tanzania (2026) Serikali Imetafakari Haya?
- Rev. Godwin Chilewa
- 2 days ago
- 4 min read
Na Rev. Godwin Chilewa

Serikali ya Tanzania kupitia GN No. 158G ya mwaka 2026 imeweka sharti la lazima kwa wafanyabiashara wa mitandaoni kuonesha wazi taarifa za kikodi kwenye profiles zao kwa lengo la “kurahisisha ukaguzi na utekelezaji.” Kwa jicho la kawaida sheria hii inaonekana kuwa na nia ya kuongeza mapato ya kodi kupitia udhibiti wa biashara za kidijitali, lakini je, serikali ilitafakari kwa kina kabla ya kupitisha sheria hiyo?
Kimsingi utekelezaji wa sheria hii una high-risk exposure katika maeneo mengi, lakini ya muhimu zaidi ni usalama wa taarifa (data security), uhalifu wa mtandaoni (cybercrime), faragha (privacy erosion) na uaminifu wa mfumo wa kodi (institutional trust). Kwa lugha ya kiintelijensia “Policy intent is fiscally rational, but operational design is strategically flawed.”
2. Mapungufu ya Kimuundo (Structural Weaknesses)
(a) Exposure ya taarifa nyeti kwenye mazingira yasiyodhibitiwa
Sheria inalazimisha kuanika hadharani namba ya kodi yaani TIN (unique identifier) na au Tax Clearance Certificate. Hizi ni ni sensitive financial identifiers, zinazopaswa kulindwa. Lakini kwa sheria hii zinahamishwa kutoka mfumo salama wa TRA kwenda kwenye Facebook, Instagram na TikTok ambako hakuna: udhibiti wa kina (access control), utawala wa data na mfuatano au rekodi ya ukaguzi. Hii ni hatari kubwa.
(b) Kukosekana kwa tafsiri sahihi ya “social media”
Sheria haijatoa ufafanuzi wa wazi kuhusu maana halisi ya biashara ya mitandaoni. Wengi wanajiuliza kama mawasiliano ya WhatsApp yanahesabiwa kama ni social media au la? Je, website binafsi ni social media? Hii inaleta utata katika utekelezaji wa sheria, matumizi mabaya ya mamlaka ta hiari, na ulengaji wa kuchagua.
(c) Kinyume na mwelekeo wa data protection
Tanzania tayari ina sheria ya Personal Data Protection Act (2022) lakini sheria hii mpya inalazimisha public disclosure ya taarifa binafsi jambo linaloleta mgongano wa kisheria. Kwa mujibu wa tathmini za haki za kidijitali, Tanzania tayari ina mazingira yenye udhibiti mkubwa wa mtandao, hofu kubwa ya ufuatiliaji, ukosefu wa uhuru wa kidijitali. Sheria hii inaongeza hali hiyo.
(d) Kutozingatia udhaifu wa mifumo ya TEHAMA
Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa mifumo mingi ya serikali Tanzania ina SQL injection vulnerabilities, XSS attacks na security gaps. Sasa serikali inataka taarifa hizo ziwekwe hadharani kwenye majukwaa yenye hatari zaidi (Rejea Usability, Accessibility and Web Security Assessment of E-government Websites in Tanzania na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) – 2024/25)
3. Tathmini ya Vitisho (Threat Assessment)
(1) Cybercrime Amplification
Utekelezaji wa sheria hii utasababisha ongezeko la wizi wa utambulisho (Identity theft ), wizi na utapeli wa kifedha, na Impersonation ya wafanyabiashara kwa kiwango cha juu. Athari ya vitendo hivi ni kubwa, na uwezekano wa kutokea ni wa hali ya juu.
(2) Uchunguzi wa Kuwalenga Wafanyabiashara fulani (Digital & Physical Threats)
Wahalifu wanaweza kufuatilia biashara kwa urahisi, Kuunganisha TIN na maeneo, Kuwalenga watu kwa wizi au unyang’anyi wa kutumia nguvu, Hili ni tushio kwa pande zote mbili, mitandaoni na hata nje ya mitandao.
(3) Zipo pia athari za kuzuia watu kutumia haki zao kutokana na hofu ya adhabu au madhara ya kuvunja sheria. Hii ni pamoja na kuzorota kwa uchumi wa kidijitali, kutokana na wafanya biashara wadogo kuogopa kujisajili. Biashara zinaweza kuhamia “underground economy”. Matokeo yake ni kupungua kwa uzingatiaji na utii wa sheria, na serikali kukosa mapato ya kodi
(4) Mitandao ya Unyonyaji wa Data (Data Exploitation Networks)
TIN za wizi zinaweza kutumika kufungua akaunti feki, kufanya miamala isiyo halali, kuhusisha watu na ukwepaji kodi au tax fraud. Zaidi ya yote mfumo wa kodi unaweza kuchafuliwa (system contamination)
4. Athari za Kimkakati (Strategic Implications)
(a) Kuporomoka kwa uaminifu wa serikali
Watu wakiona serikali inawalazimisha kuanika hadharani data nyeti wataona mfumo mzima wa kodi si salama
(b) Kudhoofisha Digital Economy Growth
Wakati dunia inaenda kwenye fintech, e-commerce, digital entrepreneurship, sheria hii inaweka friction badala ya facilitation
5. Uchambuzi wa Kiintelijensia
Kiwango cha hatari: Juu
Uwezo wa sera kudumu kwa muda : Hasi
Ufanisi wa ukusanyaji wa mapato kwa muda mrefu: Hasi”
Kwa lugha rahisi sheria inaweza kuongeza mapato kwa muda mfupi lakini kwa muda mrefu itapunguza compliance na kuharibu mfumo
6. Njia Mbadala (Strategic Alternatives)
Badala ya kulazimisha wafanyabiashara kuanika TIN, serikali inaweza kutumia njia zifuatazo:
(1) Digital Verification System (Backend Integration)
TRA iwe na mfumo wa “verification API. Platforms ziweze kuthibitisha mfanyabiashara bila kuonesha TIN. Kuwe na Verified Taxpayer Badge.
(2) QR Code System
Badala ya TIN mfanyabiashara awe na QR code ambapo TRA pekee ndio inaweza kusoma taarifa kamili. Hii itasaidia kulinda faragha na kurahisisha ukaguzi
(4) Presumptive Tax Expansion
Kama ilivyo kwenye Finance Act 2026 TRA ipanue mfumo wa kodi kwa biashara ndogo kwa kutoa tax holiday ya mwaka mmoja. Hii inahamasisha watu kuingia rasmi kwenye mfumo. Badala ya kulazimisha: itoe motisha (discounts, benefits) na ifanye compliance iwe “attractive”
Sheria hii inaashiria mambo mawili makuu: Nia ya Serikali kukusanya mapato na kudhibiti uchumi wa kidijitali. Lakini wakati huo huo haizingatii vya kutosha hatari za kiusalama wa mtandao katika uundaji wa sera. Aidha, sheria hii pia inawageuza walipa kodi kuwa vyanzo vya data vilivyo katika mazingira hatarishi na yasiyo na ulinzi wa kutosha; hivyo, badala ya kuongeza mapato kwa uendelevu, inaweza kuzalisha hatari kubwa zaidi kuliko manufaa ya mapato.
Uwe na amani.






Comments