Uchambuzi wa Kiitelijensia Kuhusu Maandamano ya 7 Julai 2026
- Rev. Godwin Chilewa
- Jul 7
- 5 min read
Updated: Jul 11
Na. Rev. Godwin Chilewa

Matukio ya Julai 7 yanaashiria mabadiliko ya kimsingi katika mienendo ya upinzani wa kijamii nchini Tanzania. Tofauti na maandamano ya jadi, tukio hili limeonyesha kuibuka kwa mkakati mpya wa upinzani usiohitaji uwepo wa watu mitaani kwa wingi bali unaolenga kuparalyze mifumo ya uchumi na utawala. Hii ni hatari kubwa zaidi kwa dola kuliko maandamano ya wazi, kwa sababu ni vigumu kudhibiti, kugundua mapema, na kukabiliana nayo kwa njia za kawaida za kiusalama.
Ni dhahiri kwamba serikali imefanikiwa katika kudhibiti physical mobilization, lakini imeshindwa kudhibiti psychological mobilization. Huu ndio ukweli wa msingi. Dola ilidhibiti barabara, lakini haikudhibiti fikra, hisia, na mitazamo ya wananchi hasa vijana.
Kwa mtazamo huu serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka za kimkakati, vinginevyo Tanzania itaingia katika mzunguko hatari wa low-intensity civil resistance unaoweza kusababisha madhara makubwa ya kiuchumi na kisiasa katika kipindi cha miaka 2 miwili hadi mitano ijayo.
1. TATHMINI YA HALI.
Tathmini inaonyesha mabadiliko ya mbinu za upinzani. Taarifa zinaonesha kuwa hakukuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu mitaani kama ilivyotarajiwa. Lakini zaidi ya 60–80% ya biashara katika maeneo ya mijini (hasa Dar es Salaam, Arusha, Mwanza) zilibaki zimefungwa kwa tahadhari. Sekta zisizo rasmi ambazo zinachangia zaidi ya 65% ya ajira nchini, zilisimama kwa kiwango kikubwa.
Hii inaashiria walioandaa maandamano wametumia mkakati wa Decentralized protest, Economic shutdown strategy, na Fear-induced compliance. Huu ni mfumo wa upinzani unaofanana na ule uliotumika katika nchi kama Sudan (2019) na Kenya (2023), ambapo maandamano yalibadilika kutoka mitaani kwenda katika kuvuruga mifumo ya uchumi. Kwa ujumla kiusalama hatari iko juu (High Risk Evolution).
1.2 Athari za Kiuchumi (Rapid Impact Indicators)
Kwa kutumia makadirio ya msingi ya uchumi Tanzania hupata wastani wa zaidi ya TZS trilioni 1.3 hadi 1.5 kwa siku katika shughuli za kiuchumi (GDP per day estimate). Kusimama kwa shughuli hata kwa asilimia 30–40% kunamaanisha hasara ya moja kwa moja ya takribani TZS bilioni 400–600 kwa siku.
Sekta ya utalii inayoingiza zaidi ya dola bilioni 2.6 kwa mwaka iko katika hatari ya kupoteza bookings kutokana na hisia za nchi kutokuwa salama au madhubuti (perception of instability). Pia zipo athari zisizo za moja kwa moja kama kuongezeka kwa country risk perception. Kupungua kwa uwekezaji wa muda mfupi (short-term capital hesitation) na kuathirika kwa mapato ya kodi (TRA collections disruption). Zingatia kwamba hasara si tukio la siku moja ni signal kwa masoko ya kimataifa.
1.3 Tathmini ya Kisaikolojia na Kijamii (Psychological Terrain Analysis)
Uchambuzi unaonesha kwamba sasa Vijana (GEN Z) hawana hofu ya moja kwa moja ya dola, bali wanatumia strategic avoidance. Kuna kuongezeka kwa hali ya upinzani wa kimya kimya (silent dissent). Mitandao ya kijamii imekuwa chombo kikuu cha uratibu usio rasmi (informal command structure).
Hali hii ni hatari zaidi kuliko maandamano ya wazi kwa sababu upinzani au maandamano haya hayana viongozi wa wazi (leaderless resistance), ushawishi wake hauwezi kukatwa kirahisi kwa kukamata watu wachache, na hatari ina uwezo wa kujirudia bila maandalizi makubwa
Tathmini inaonyesha kuwa mfumo wa upinzani umeingia hatua ya “adaptive intelligence”.
2. MAKOSA YA KIMKAKATI YA SERIKALI
2.1 Utegemezi Uliopitiliza wa Udhibiti wa Kulazimisha (Coercive Control)
Serikali imewekeza zaidi katika kudhibiti dalili (symptoms) badala ya chanzo (root causes). Hii ni mbinu ya muda mfupi. Ni sawa na kumpa mgonjwa wa jino dawa ya kutuliza maumivu badala ya kuling’oa jino bovu.
2.2 Kudharau Uwezo wa Vijana
Tathmini inaonyesha serikali inadharau uwezo wa vijana katika kupanga na kuratibu upinzani bila muundo rasmi. Hili ni kosa kubwa la kiintelijensia. Hivi sasa vijana wana mtandao mkubwa uliojipenyeza mpaka ndani ya serikali. Wengi wa Gen Z wanataka mabadiliko.
2.3 Kushindwa Kudhibiti Simulizi
Serikali haijafanikiwa kudhibiti simulizi (narrative). Vijana wamechukua nafasi hiyo na kugeuza tukio kuwa “ushindi wao wa kimkakati.” Zingatia kwamba lengo la vijana ni kudai haki kwa kuionesha dunia kwamba mfumo uliopo nchini unakandamiza haki na demokrasia.
2.4 Pengo la Kiitelijensia (Soft Intelligence Failure)
Ingawa taarifa za moja kwa moja (hard inteligence) kama uwepo wa vikundi au viongozi wanaoratibu tukio, taarifa za vitisho, maandalizi ya maandamano na vikundi vilivyojaribu kugamasisha vurugu, mienendo ya watu maeneo fulani na nambo mengine ya kiusalama zilikuwa nzuri, taarifa kuhusu hali ya ndani ya jamii kama hisia, mawazo na mwelekeo wa wananchi zilikuwa dhaifu.
Tathmini inaonesha serikali bado haijatilia maanani saikolojia ya jamii hususan wananchi wanafikiria nini kuhusu serikali, kiwango cha hasira au kukata tamaa kwa jamii, malalamiko yanayoenea, mijadala kwenye mitandao ya kijamii, mabadiliko ya maoni ya watu, na sababu za kweli zinazoweza kuwafanya watu waunge mkono au kupinga jambo fulani.
Viongozi wa kitaifa bado wana mtazamo kwamba upinzani, maandamano na kiu ya mabadiliko ya mfumo ni matokeo ya ushawishi na hujuma za mataifa ya nje, na kwamba vijana wamenunuliwa au hulipwa fedha ili kuchochea fikra za mabadiliko. Dhana hii ni potofu na inachelewesha au kuzuia ufumbuzi wa kweli wa tatizo husika.
3. HATARI ZA BAADAYE
Ikiwa hali hii itaachwa kuendelea bila mabadiliko mambo yafuatayo yanaweza kutokea: Katika kipindi cha miezi 6 hadi 12 hali itakuwa tete zaidi. Kuongezeka kwa “stay-at-home protests” kutasababisha kuyumba kwa uchumi na kuathiri mzunguko wa fedha mijini
Ndani ya mwaka 1 hadi 3 taifa litakumbwa na kupungua kwa imani ya wawekezaji, kutakuwa na ongezeko la migogoro ya kijamii ya chini kwa chini (latent instability) na uwezekano wa milipuko mikubwa zaidi ya kisiasa, na ndani ya miaka 5 nchi inaweza kuingia katika hali ya stagnation under uncertainty
4. MAPENDEKEZO YA KIITELIJENSIA
4.1 Shift kutoka Coercion kwenda Engagement
Serikali lazima ibadilishe mkakati wake kutoka “control model” kwenda “engagement model” kwa maana ya kuondoa udhibiti kwenda kwenye kujenga mawasiliano, ushirikiano na uaminifu, na iache kusimamia zaidi usalama wa kimwili kuliko sababu zinazosababisha watu kutoridhika.
Kwa sasa serikali inachukulia malalamiko ya wananchi kama tatizo la kiusalama badala ya ujumbe wa kisiasa au kijamii unaohitaji kusikilizwa. Hili lizingatiwe kwa umakini na kwa kuimarisha majukwaa halisi ya kusikiliza vijana
4.2 Kuanzisha Mifumo Ramsi ya Kukusanya Maoni ya Wananchi (structured civic feedback systems)
Kwa Sasa kazi ya kukusanya taarifa na maoni ya wananchi hufanywa na vyombo vya dola, hususan TISS. Aidha viongozi wa serikali kama waziri mkuu na wakuu wa mikoa na wilaya huzunguka kusikiliza na kutatua migogoro. Lakini bado inapaswa kuanzisha na kutumia mifumo rasmi ya kukusanya maoni ya wananchi. Intelligence iwe sio ya usalama tu, bali ya kijamii (social intelligence)
Katika nchi nyingine vyombo vya habari huisaidia serikali kufanya kazi hii kwa kuandika kwa usahihi malalamiko, hisia za wananchi, na makosa ya serikali kama yapo. Tanzania jambo hili limekuwa gumu kutokana na kukomaa kwa uchawa, na vitisho vya serikali dhidi ya vyombo vya habari au watu wanaoikosoa serikali. Hili hufanya Rais na serikali yake kukosa taarifa sahihi za hisia za wananchi.
4.3 Kupunguza Hali Ngumu ya Maisha.
Hatua za haraka zichukuliwe kupunguza shinikizo la maisha (cost of living interventions). Hii ni pamoja na kuangalia upya vyanzo vya mapato ya serikali ili kuweza kupunguza utitili wa ushuru, kodi , na tozo zinazomkabili mwananchi wa kawaida. Aidha serikali ianzishe Programu za ajira kwa vijana zenye matokeo yanayoonekana.
4.4 Strategic Communication Reset
Serikali irejeshe uaminifu kwa uwazi na consistency na kwa kudhibiti narrative kwa ukweli, si propaganda. Serikali irejee kwenye mfumo wa utendaji wa Rais Benjamin Mkapa uliosisitiza ukweli na uwazi.
4.5 Ifanyike Intelligence Reform
Hili ni muhimu sana hasa kwa kipindi tulichonacho. Idara inapaswa kuwa na wachambuzi nguli wenye predictive intelligence, na wenye uwezo wa kuchambua na kuunganisha taarifa za kiuchumi, kijamii, kiusalama na kisiasa katika uchambuzi mmoja
5. ONYO LA KIITELIJENSIA
Julai 7 si mwisho wa maandamano au matukio, ni mwanzo wa awamu mpya. Serikali ilishinda vita ya barabarani, lakini imeshindwa katika vita ya kisaikolojia na kiuchumi. Hii ni hatari zaidi.
Historia inaonyesha wazi kwamba dola zinazoshindwa kusoma ishara ndogo za mwanzo (early warning signals) huishia kukabiliwa na migogoro mikubwa isiyodhibitika.
Ni dhahiri kuwa kama serikali ikidharau kushughulikia mizizi ya tatizo, Tanzania itaingia kwenye mfumo wa upinzani wa kimya unaoweza kuumiza uchumi na uthabiti wa taifa kwa muda mrefu zaidi kuliko maandamano ya wazi. Kumbe viongozi wana hiari ya kurekebisha mfumo sasa au kulazimishwa kurekebisha kwa gharama kubwa zaidi baadaye.
Uwe na amani






Comments