top of page

Viaticum - Sakramenti ya Mwisho

Mwaka 1990 Papa Yohane Paulo wa pili alifanya ziara ya kiserikali nchini Tanzania kufuatia mualiko wa rais Ali Hassan Mwinyi. Ziara hiyo ilisifiwa na wapenda amani duniani kote kwa kuleta umoja na kuwaunganisha watu wa dini na imani mbalimbali barani Afrika. Zaidi ya miaka 30 baadae ndipo inapobainika kwamba ziara hiyo ilikuwa na ajenda nyingine kubwa na ya siri siri kuu. Siri inayoweza kusambaratisha kanisa katoliki, na kusababisha umwagaji mkubwa wa damu. Ni katika sintofahamu hiyo Eddy Kashe, mwandishi wa habari za uchunguzi anapojikuta akipewa kazi na mtu asiyejulikana. Kazi ya kuutafuta ukweli na kurudisha amani na heshima ya nchi. Kupata uhondo wa riwaya hii bofya linki ya kujiunga.



Comments


bottom of page